Wizara ya Maji kuwajengea uwezo wahandisi wake, yaahidi makubwa kutatua changamoto za maji nchini - Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

top+logo

"Muda Unaongea"

Breaking

Home Top Ad

jiachie

Post Top Ad

27 Jun 2019

demo-image

Wizara ya Maji kuwajengea uwezo wahandisi wake, yaahidi makubwa kutatua changamoto za maji nchini

jiachie
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amesema wizara imepanga utaratibu maalum wa kuwajengea uwezo wahandisi wake kiutendaji na kitaaluma kwa lengo la kuleta mabadiliko yanye tija katika Sekta ya Maji.
65809069_1169007220137748_7975299143872544768_o.jpg?_nc_cat=105&_nc_oc=AQmMQGBfP6A8c-4V6YR37bDYh9-i4sXJumqVelqx4OmRlxdwTn1y7Ut5580ipc3lzLs&_nc_ht=scontent.fzag1-1
Profesa Mkumbo ametoa kauli hiyo katika kikao na watumishi wa Idara ya Usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira (DWSS) katika maadhimisho ya Wiki wa Utumishi wa Umma kilichofanyika katika Ukumbi wa DUWASA.
"Ili tuweze kupiga hatua katika utekelezaji wa miradi, tumeandaa mfumo mzuri wa kuwajengea uwezo wahandisi wetu ili waweze kuwa na ujuzi mkubwa katika majukumu yao na kuanzia mwaka ujao wa fedha tutaanza kuutekeleza", Profesa Mkumbo ameahidi.
"Tunataka kuwa na timu ya wahandisi wazuri kwenye Sekta ya Maji watakaosimamia miradi yetu ya maji kwa mafanikio na tumetenga fedha kufanikisha zoezi hilo", Profesa Mkumbo amesisitiza.
65188670_1169007210137749_259786353938530304_o.jpg?_nc_cat=101&_nc_oc=AQntFtbOJYvhGtXrDDbeKAvWrmroLcZgtwHFsDEJgPAWzs5o4sNHpqOkVQCjoPOm5hU&_nc_ht=scontent.fzag1-1
Akizungumza kwenye kikao hicho Profesa Mkumbo amesisitiza kuwa wizara itakuwa na utaratibu mahsusi wa kuwasaidia wahandisi wachanga kupata usajili kwenye Bodi ya Wahandisi (ERB) na akiahidi mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa Mamlaka za Maji pamoja na usimamizi mzuri wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) utakaoanza Julai Mosi, 2019, akiwataka watumishi hao wafanye kazi kwa bidii wakiiachia wizara jukumu la kuboresha mazingira yao ya kazi katika ngazi zote.

Pia, akionya kuwa hakutakuwa na nafasi kwa wahandisi wazembe na wasio waadilifu kwa kuwa hawatafanya kazi katika Wizara ya Maji.
65287717_1169007206804416_7110931774347149312_o.jpg?_nc_cat=103&_nc_oc=AQkCWyaBqEbR-mFHbh9k4xysmhiUqDNKDQ9An-yQ_BXQ_z4aizii3mHXmWT08th7HtE&_nc_ht=scontent.fzag1-1
Akitoa shukrani zake kwa Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira, Mhandisi Nadhifa Kemikimba amemshukuru Profesa Mkumbo kwa kutenga muda wa kukutana na kuwasikiliza watumishi wa idara yake.
Mhandisi Kemikimba pia akawasuhi watumishi hao kuongeza juhudi katika kazi kwa kuwa idara hiyo ndiyo imebeba dira na lengo la wizara kwa asilimia kubwa.
Dhumuni la kukutana na watumishi hao lilikuwa ni kusikiliza changamoto zao kwa lengo la kuzifanyia kazi katika kuhakikisha kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji inaongezeka na kuinua kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji kwa watanzania.

Imeandaliwa na Wizara ya Maji

Post Bottom Ad

Pages