___________
Francis Daudi
Wizara ya fedha kwa Tanzania inachukuliwa kama wizara nyeti zaidi katika nchi yetu ya Tanzania hasa kwa kuwa husimamia mgawanyo wa fedha kwa matumizi yote ya serikali, pia inasimamia miradi na taasisi zote za kifedha. Inasimamia pia hazina almaarufu ‘kibubu cha Taifa’
Ni hivi Sir Ernest Albert Vassey(kwa sasa ni marehemu) alikuwa waziri wa kwanza wa fedha na mipango kuanzia mwaka 1960 mpaka 1962 alipomwachia mzalendo Paul Bomani (kwa sasa ni marehemu).
Ernest Vassey alizaliwa mwaka 1901 Maryport, Cumberland, Uingereza. Alifika Kenya kama mwanasiasa kijana akawa diwani wa eneo la Westland katika Halmashauri ya Manispaa ya Nairobi.
Akiendelea kuimarika katika siasa, hatimaye akawa Meya wa Jiji la Nairobi kati mwaka 1941-1942 na 1944-1946.
Alihamia Tanganyika na kuwa Waziri wa Fedha na Mipango tangu 1959-1960, Alikuwa rafiki mkubwa wa Mwl.Jk Nyerere kwani aliunga mkono harakati za Watanganyika kuwa huru, Hivyo baada ya Nchi kupata uhuru wake Nyerere alimrudisha katika wizara hiyo hiyo kama waziri wa kwanza Fedha na Mipango wa Tanganyika huru.
Alihamia Tanganyika na kuwa Waziri wa Fedha na Mipango tangu 1959-1960, Alikuwa rafiki mkubwa wa Mwl.Jk Nyerere kwani aliunga mkono harakati za Watanganyika kuwa huru, Hivyo baada ya Nchi kupata uhuru wake Nyerere alimrudisha katika wizara hiyo hiyo kama waziri wa kwanza Fedha na Mipango wa Tanganyika huru.
Alichangia sana katika kujenga misingi na taratibu za kifedha zinazotumika hata sasa katika wizara hiyo, Mawazo yake yamekuwa ndio chachu za uanzishwaji wa taasisi za elimu ya fedha na biashara hapa Tanzania.
Mwaka 1962 alijiuzulu uwaziri huo ambao alipewa na Mwl.Jk Nyerere kutokana na chuki ya wanachama wa chama Tawala wakati huo TANU ambao hawakupenda nafasi hi hiyo nyeti kupewa mtu kutoka nchi za nje ,alijiuzulu na kumuachia nafasi ndugu Paul Bomani lakini akakubali cheo cha mshauri mkuu wa maswala ya fedha Tanganyika lakini akiendelea kupata mshahara ule ule wa uwaziri hadi mwaka 1966.
Baadaye akafanya kazi za masuala ya fedha huko Pakistan kwa miezi kadhaa na kurejea Kenya na kujikita katika kusimamia jengo la sinema(Ilikuwa kazi yake ya ujana).
Francis Daudi, Melukote!