Tukio la Lissu kupigwa risasi jinsi linavyochukuliwa kisiasa kutafuta uungwaji mkono - Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

"Muda Unaongea"

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

25 Jun 2019

Tukio la Lissu kupigwa risasi jinsi linavyochukuliwa kisiasa kutafuta uungwaji mkono



Wakati fulani Waziri Mkuu wa Sweden Olof Palme na mkewe Bi Lisbet walikuwa Mitaa ya Sveavägen katikati ya Stockholm wakitokea kutazama filamu bila ya walinzi, Ghafla! alitokea mtu kwa nyuma na kumpiga risasi moja. Palme alikimbizwa hospitali na kuthibitika kuwa amefariki Dunia.

Kwa nchi kama Sweden iliyokuwa(inayo hata Leo) na utulivu mkubwa wa kisiasa tukio hilo liliishtua Dunia. Inaelezwa majira ya saa 5 na dakika 21 usiku (Saa za Sweden) ilikuwa Ijumaa tarehe 28 Februari 1986, Palme alikuwa akitembea na mkewe wakiwa huru tu. Ndipo alipopigwa Risasi moja na ingine ikamjeruhi mkewe!

Tangu 1986 hadi Leo, watu takribani 10,000 wameshahojiwa juu ya tukio hilo. Hakuna aliyethibitika hasa kuwa ndiye Muuaji wa Palme. Mke wa Palme, Bi Lisbet alimtambua Christer Petterson kama Muuaji na Mahakama ilimuhukumu kwenda jela Maisha. Lakini ushaidi uliokusanywa baadae ulithibisha pasi na shaka Lisbet alimtambua kimakosa Petterson. 

Hivyo basi Petterson alilipwa fidia ya dola elfu 50. Na vyombo vya Usalama Sweden mpaka Leo vinakusanya taarifa za kifo cha Palme. Petterson alitumia fidia hiyo kwa Ulevi na anasa zingine.

Imeandikwa na Francis Daudi

Post Bottom Ad