CHADEMA na mchezo wa kuwatelekeza wanachama wake na ahadi hewa kwa wananchi - Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

"Muda Unaongea"

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

25 Jun 2019

CHADEMA na mchezo wa kuwatelekeza wanachama wake na ahadi hewa kwa wananchi

Anaandika Bollen Ngetti
FULEGENCE Mapunda al-maarufu Mwanakotide si wa kwanza kutelekezwa na Chadema. Wako wengi na ninaambiwa na wana Chadema wenyewe kuna ubaguzi mkubwa ndani ya Chadema katika matatizo.
Chadema imemtelekeza mke wa David Mwangosi waliyeahidi kumsomeshea watoto. Mjane analia na kusaga meno! Haamini macho yake kama kweli huyu ni Mbowe au mbawa!
Chadema imemtelekeza Msafiri Mbwambo. Kubwa kuliko zote Chadema kwa makusudi imetelekeza familia ya Alphonce Mawazo. Inauma sana.
Pamoja na ukweli kuwa Ben Sanane alikuwa msaidizi wa Mbowe lakini Baba Mzazi wa Ben alizilalamikia mamlaka za CHADEMA kwa kushindwa kufika hata nyumbani kwake kujua kuhusu kijana wake Ben zaidi ya kupiga makelele katika mitandao ya kijamii jambo alilosema kuwa kama familia hawaoni umuhimu wake.
Tarehe 30/11/2015 siku ya mazishi ya Mawazo Freeman Mbowe alitangaza hadharani kwamba wabunge wa Chadema na Ukawa kwa ujumla wamechanga Shilingi 33 milioni taslimu na watamkabidhi mke wa Mawazo.
Hadi leo fedha hizo hazijulikani zimekwamia wapi. Wengine wanasema zimekarabati ofisi ya chama makao makuu. Mbowe kimya.
Waliahidi kujenga kaburi la Mawazo ikawa ni hewa hadi familia na marafiki wakachangishana kujenga kaburi hilo na sanamu yake!
Freeman Mbowe, wewe ni kaka yangu, ni rafiki yangu, ni shemeji yangu, tunakula na kunywa pamoja lakini kwenye hili la kutelekeza watu nasema NO. Acha kabisa utapeli huu. Hebu mpelekee mke wa Mawazo 33m zake! Ikiwezekana iwe leo! Kesho nitakuuliza ukija Manzese labda uingie mitini!.

Post Bottom Ad