Dr. Mashinji kupitia ukurasa wake wa twitter amewatia wachezaji wa Timu ya Tanzania iliyocheza mchezo wa jana dhidi ya Kenya-Harambee Stars baada ya matokeo ya mechi hiyo kuisha kwa Tanzania kuzidiwa nguvu na Kenya kwa goli tatu kwa mbili. Katika mchezo huo zimeibuka kauli zenye kuonyesha dharau na lawama kwa timu ya taifa kutoka kwa vijana mbalimbali ambao wengi wao wameonekana kuwa na mahaba zaidi ya kisiasa kuliko michezo. Ambapo amewataka watu wote wanaoongea maneno ya kuwabeza na ubaguzi na kuwaambia kuwa wao ni timu ya taifa na wanaliwakilisha taifa.
Taifa Stars: hongera kwa kujituma kutetea Taifa na pole kwa kukosa matokeo tarajiwa uwanjani.— Dr. Vincent Mashinji (@Vicent_mashinji) June 28, 2019
Tunajivunia kuwa nanyi. Taifa litaendelea kuziba mapengo yaliyojitokeza.
Puuzeni maneno ya kibaguzi ambayo baadhi ya vijana wetu wameyasema juu yenu.
Ninyi ni TIMU YA TAIFA! pic.twitter.com/Mkn8KZOekk