Vijana leo mmejitahidi kadri ya uwezo wenu na kadri ya maandalizi mliyopewa na nchi yenu kucheza mpira mzuri sana, magori yaliyopatikana ni matokeo tu. Kila aliyetazama mpira wa leo amefarijika jinsi vijana wetu walivyoonyesha uwezo mzuri ktk kushiriki haya mashindano baada ya nchi yetu kushindwa kufuzu kushiriki mashindano haya kwa takribani miaka 40.
Ninachoweza kusema ni kuwa, WAHUSIKA wakihusika ipasavyo, Tanzania inaweza kuwa na timu nzuri sana itakayoleta ushindani AFCON miaka 20 mpaka 30 ijayo. Hongera sana kapteni Mbwana Samatta kwa kujitoa kufa kupona dhidi ya Tanzania kwa kuhakikisha bendera yetu inapepea kila kona ya dunia.

Magoiga SN