Hawa ni ndege wanaopatikana sehemu kubwa ya dunia, ni ndege maarufu sana kutokana na tabia yao ya kukaa wengi kwenye kundi moja.
Flamingo ni neno lililotoka katika Nchi ya Hispania "FLEMINCO" likimaanisha "MOTO" na hii ni kutokana na manyoya yao kuwa na rangi ya bright pink na orange.
Wamegawanyika katika jamii sita (species), baadhi hupatikana hapa Africa na nyingine hupatikana mabara mengine. Wanaopatikana hapa Africa wanaitwa "LESSER FLAMINGO na GRATER FLAMINGO".
Ukubwa wao umetofautiana kutokana na species lakini kawaida huwa na urefu kuanzia futi 2.9 - 4.8 na uzito wao huwa ni kg 2.5 mpaka kg 4 na mabawa yao huwa na urefu wa cm 150
.
Kawaida flamingo hawana asili ya rangi ya orange na bright pink, huzaliwa weupe. Rangi ya pink na orange hutokana na chakula wanachokula ambacho huwafanya kawa na ile rangi. Wanakula pigments zinazopatikana kwenye algae pamoja na invertebrate animals (wale minyoo na vunja chungu, hvi huyu vunja chungu kwanini aliitwa hili jina? 😀).
Ndege hawa wanaishi zaidi majini kuliko ndege wengine. Hutegemea sana maji kwa ajili ya miili yao hivyo hupatikana zaidi kwenye mabwawa na maziwa
Flamingo ni non-migratory yaani sio ndege wanaohama hama mara nyingi huwa na makazi ya kudumu
.
Flamingo ni omnivores wanakula majani lakini pia wanakula nyamaa mfano wanakula sana samaki wadogo na baadhi ya wadudu.
Chakula wanachokula hutegemea sana na aina ya flamingo na mdomo wake ulivyo. Baadhi hula sana algae na wengine hula sana wadudu.
Adui wao mkuu ni eagle pamoja na nyani (hivi nyani hawali nini yaani jamaa kama wachina vile kila kitu wanakula😀😀)
Wanaishi kijamii sana na kwenye kundi moja wanaweza kufikia mia moja.Jukumu la ulinzi ni la kila mmoja kumlinda mwenzake ili asiliwe
Kwenye group huwa na madume kadhaa ambayo huwa na vita kidogo katika kutafuta mubebe na hawanaga michepuko akishapata bebi wanatulia wanakula bata na kuangalia wavuvii tu (muda wote wako vacation)
Majike yote hutaga kwa muda mmoja, hutaga yai moja au mawili pembezoni mwa ziwa na huanguliwa baada ya siku 31 na watoto huwa ni weupe
Ndege aina ya flamingo wanaishi hadi kufikia miaka 50.
CC Hilary Silayo
#UnforgettableTanzania #TanzaniaTourism #TanzaniaWildlife