Kigoma tulifanya makosa 2015 - Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

"Muda Unaongea"

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

17 Jul 2019

Kigoma tulifanya makosa 2015

KIGOMA TULIFANYA MAKOSA 2015. MSOME Abdallah Mtonda


Nikiwa kama kijana wa Manispaa ya Kigoma Ujiji sijaendezwa hata Kidogo na sheria ambazo zinaenda kupitishwa muda sio mrefu na viongozi waliopata dhamana ya kutuongoza kwa Miaka 5 ACT.

Sheria hizi zikipititishwa zitakuwa hazina afya na zitapekekea uchumi wa miji wetu kushuka, badala manispaa kuwapunguzia mzigo wakazi wake iliwapande kiuchumi, wao ndio kwanza wanataka kuwanyonya na kuwadidimiza ili wasiiunuke kabisa.

Yako mengi ambayo wanaenda kuyapitisha ili kumkamua mwananchi wa kawaida na asichomeke, leo unasema hawa watu wanaitakia mema Manispaa ya Kigoma Ujiji serious kwa madudu haya.

ACT yaani kabisa mnataka kuwakamua hadi wapiga picha ambao wamejiajiri na wanajiingizia kipato chao na wengine wanafamilia kiasi cha Tsh 50,000 kwa mwezi. Au lengo lenu ni kuwafanya waache kazi hiyo.

Wacheza Ludo na michezo mingine ya namna hiyo kama Draft, Zuna na pool table na wao mnataka kuwa kamua kila mwezi na wao wawe wanatoa ushuru kiasi cha Tsh30,000.

Naona ushuru wa mazao yatokanayo na mifugo pia mmekaba hadi kipa wanaofanya biashara hiyo mmejiridhisha wanauwezo kiasi gani au ndio tu kujipatia mapato hata kama watu wanaumia.

Pia, kuna ushuru kwa wanaoingiza mazao yatokanayo na mbao, kama nawaona wachonga meza, makabati na viti wakipandisha bei bidhaa zao.

Kuna Tozo kwa ajili ya harusi hapo naona ni Tsh 40,000 .

Kuhusu ushuru wa masoko wa Tsh 300 Mh, Raisi ameshawaambia wafanya biashara wakate vitambulisho. Kikubwa mnapaswa kuwahimiza wafanya biashara wakakate vitambulisho hayo ya 300 kila siku hayawahusu.

Kikubwa zaidi mliaminiwa na wnanakigoma fanyeni kazi kwa kuwaletea maendeleo na sio kuwa kamua wananchi.

Tunasema Kupanga ni Kuchagua.

Mwananchi wa Kawaida
Abdallah Mtonda
4/7/2019
Kigoma Tanzani.

Post Bottom Ad