Na, Francis Daudi.
Umewahi kukuta tangazo la kazi alafu maelekezo ni kuwa barua ya maombi iandikwe kwa mkono?
Umewahi kuona mtu anaandika mwandiko mkubwa? Mwingine mdogo sana?
Jinsi unavyoandika unaweza kueleza juu ya uwezekano wa wewe kuwa na shinikizo la damu, msumbufu, mcheshi, mwaminifu, mchoyo na mwenye busara.
Taaluma ya grafolojia imetumika na wanasaikolojia katika kutambua hali za watu mbali mbali katika dunia tangu miaka ya 1622 huko nchini Ufaransa.
Tuangalie mifano ifuatayo;
- Watu wenye miandiko mikubwa kwa kawaida hupenda sana kujaliwa, hupenda kujichanganya na jamii na ni wacheshi mno.
- Watu wenye miandiko midogo kwa kawaida ni watu wenye aibu, wenye umakini wa hali ya juu na mara nyingi uwa ni watu wapole na wasikivu.
- Kama mtu huacha nafasi kubwa kati ya neno na neno kwenye sentensi basi mtu huyo anapenda kuwa huru, hapendi milolongo mirefu na pia hueshimu uhuru wa mtu mwingine kujifanyia mambo.
- Kama mtu huacha nafasi ndogo kati ya neno na neno kwenye sentensi basi mtu huyo hawezi kujitegemea mwenyewe hasa kimaamuzi, kimawazo na mara nyingi uwa na hasira za ghafla.
- Watu wenye miandiko ambayo herufi huungana wakati wakiandika kuna uwezekano watu hao ni wenye mantiki ya juu katika kuzungumza, uwa ni viongozi na wapenda haki.
- Watu wenye miandiko ya herufi zinazokuwa kama mviringo na zinazoachana(Kila silabi na konsonanti inaonekana bila kugusana au kuungana) uwa ni watu wabunifu, waaminifu na wenye akili sana.
- Mwandiko wa kukandamiza kiandikio huashiria mwandishi ni mtu anayechukulia kila kitu kwa umakini pia sio watu wa kuyumbishwa hasa katika maeneo ya kazi na kiuongozi.
- Miandiko isiyokolezwa yaani asiyetumia nguvu katika kuandika huashiria mtu huyo ni mpoteza muda, asiyejali sana na hapendi kuendeshwa na hisia zake.
- Watu wanaoandika haraka ni watu wasio wavumilivu, hawana subira na mara nyingi hutaka vitu view vile wanavyotaka wao bila kuangalia athari zake.
- Watu wanaoandika taratibu ni wenye kupenda kwa dhati, wavumilivu, wenye mipangilio lakini mara nyingi ni wachoyo mno.
