1. Hatujasikia CHADEMA wakitenga siku ya kuwaenzi Mtei na Bob Makani wala CUF kumuenzi Seifu na Mapalala. Hata huko ACT hakuna mwelekeo watakumbuka hili. Ikiwa mnashindwa kuwaenzi waasisi wenu mtaweza kumuenzi mwalimu, kawawa na wenzao tukiwapa nchi? Hamuoni huu ni udhaifu?

2. Hatujawasikia mkikumbuka siku vyama vyenu vilipozaliwa. Yaani hata watu hufanya birthday zao nyie mmesahau ya vyama vyenu? Au hamkumbuki vilizaliwa lini? Tukiwapa nchi mtakumbuka kuzaliwa Kwa Taifa la Tanzania? Hivi kama hamuenzi historia ya vyama vyenu mtaenzi historia za kitaifa?
3. Toka 1985 viongozi ni walewale. Mtoto aliyezaliwa 1985 ni kijana mkubwa Tu. Hivi kweli mkipewa madaraka ya kuongoza kina Mbatia, Mbowe, Rungwe, Zitto mtakubali kuondoka Ikulu? Yaani hata kuwaza lini mtaondoka kuongoza vyama muwapishe wengine inakuwa taabu? Huu si ndio udikteta? Hivi ukienda Ulaya kudai Tanzania kuna udikteta wakakuuliza kwani eti wewe uko hicho cheo toka lini si utaonekana chizi?
4. Hivi mtu mzima tena mwanaume akashindwa kujijengea makazi ya kueleweka wakati anaonekana kilabuni anatoa ofa ataaminika? Hivi Kwa nini hamna ofisi zenye hadhi? Ruzuki mnapewa, wanachama mnao wanalipa Ada, wabunge mnao wanakula posho, wafadhili nje mnao, sabodo alikuwepo bado ofisi hamna? Tutawaamini vipi? Mnapata hela ya kuzurura Ulaya kutukana mnashindwa kujenga ofisi walau kila mkoa?
5. Hivi huko kwenye vyama vyenu kila mmoja ana ndevu? NI kambale mtoni? Inakuwaje kila mmoja anajisemea anavyotaka? Kila anayetaka kuitisha press anaitisha! Tukiwapa nchi si itakuwa shughuli? Kila mmoja anawahi mic?
Kwa leo naishia hapa lakini mjue adui yenu ni nyie wenyewe. Hawa wananchi mnaodhani hawajui kitu wana akili sana! Wanajua kuchambua pumba na mchele. Wanamuona mpinzani wenu anavyofanya mambo kwa makini. Wanamuenzi muasisi wao kila oktoba, wanasherehekea kuzaliwa kwa chama chao, wana msemaji maalum, ofisi ziko kila ngazi na wana utaratibu unaoeleweka wa kubadili viongozi.
Tatizo mmejipachika uharakati! Mngemsikia Lowasa mngepona!..
#Note: Pichani ni Muasisi wa Chadema, Mzee Edwin Mtei (Baba Mkwe wa Mbowe). ✌
Wasalaam!.