Taarifa ya kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma (PAC), imesema kuwa shirika la hifadhi ya jamii NSSF limefanya uwekezaji usio na tija katika ununuzi wa ardhi maeneo kadhaa nchini huku taarifa hiyo ikifichua madudu yaliyofichwa na kamati hiyo kwa zaidi ya miaka 8 sasa kipindi chote ilipokuwa ikiongozwa na Zitto Kabwe (2008 - 2015)
Pamoja na madudu mengi yaliyoibuliwa na kamati hiyo ambayo huko awali yalifichwa , Bunge leo limearifiwa kuwa shirika hilo lilipata kununua jumla ya heka 28 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.85 sawa na shilingi milioni 66 kwa heka kijijini Mwandiga wilayani Kigoma jimbo la Kigoma kaskazini jimbo lililokuwa likiongozwa na mbunge Zitto Kabwe kuanzia mwaka 2005 hadi 2015 ambaye miaka mitatu tu tangu kuchaguliwa kuwa mbunge alichaguliwa pia kuwa mwenyekiti wa kamati ya POAC na baadae PAC
Katika hali ya kustahajabisha ni kwa namna gani NSSF iliyokuwa ikiongozwa na Dkt. Ramadhani DAU iliweza kujiingiza kichwakichwa kukubali kushawishiwa kushiriki katika mradi huo usio kuwa na kichwa wala miguu mradi wa ujenzi wa ‘MWANDIGA TRANSPORT TERMINAL’ mradi uliopangwa kugharimu jumla ya shilingi bilioni 33.3 zinazotokana na michango wa watanzania wanaotunza fedha zao.
Katika hali ya kustaajabisha, mara zote haijawahi kutokea popote mwenyekiti wa kamati hiyo wa kipindi hicho Zitto Kabwe akikemea hata kwa kudanganya uwekezaji mbovu usiofaa wa namna hiyo kwa shirika hilo kubwa na muhimu nchini
Taarifa za uhakika zinasema bei ya sasa ya heka moja ya shamba wilayani Kigoma katika eneo la mwandiga ni kati ya shilingi laki tatu hadi milioni mbili jambo linaloshangaza zitto kuishawishi NSSF ya DAU kununua Shamba heka moja milioni 66.
Miradi mingine ambayo NSSF imeliingiza hasara shirika hilo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Apollo ya jijini Dar es salaam ambao hadi hivi sasa umeshatumia bbilioni 4.19 huku mkandarasi akiwa amekimbia site.
Mradi mwingine ni ule wa ujenzi wa jingo la ubalozi na biashara vwenye thamani ya bilioni 77, mradi wa kuzalisha umeme mkuranga (mkuranga power generation) wenye thamani ya shilingin Trilion 1.15, mradi wa ujenzi wa nyumba katika eneo la kiseke na bugarika mkoani Mwanza ulioanza kutekelezwa mwaka 2008 hadi leo haujakamirika wala hautarajii kukamilika na tayari maeneo yameshavamiwa na wananchi huku zaidi ya shilingi bilioni 1.51 zikiwa zimetumika.
Mradi mwingine ulioasisiwa na NSSF ya Dkt. Dau iliyokuwa ikikaguliwa na PAC ya Swahiba wake Zitto kabwe ni mradi wa ujenzi wa nyumba katika plot namba 249 njiro mkoani Arusha mradi uliogharimu shilingi bilioni 14.7
Aidha manunuzi ya ARDHI katika mikoa ya Pwani na Dar es salaam ambapo NSSF walitumia jumla ya shilingi bilioni 15.8 kununua plot 5 katika mikoa ya Dar na Pwani ambapo kiasi hicho cha fedha kilitumika kununua ardhi jiyo bila kufanyika upembuzi wa kina wa miradi iliyotakiwa kutekelezwa na shirika.
Kamati ya PAC pia imebaini kuwa jumla ya shilingi bilioni 27.1 ambazo ni mali ya wananchama zipo hatarini kupotea kwa sababu ya maamuzi ya uwekezaji usiokuwa na tija.
