Najua wananchi wengi wanashindwa kuelewa mambo aya ambao sisi tumeamua kusema ni Uchuro au uchimvi.

Watanzania kwa ujumla tumezoea kuona uovu au uchafu wa Serikali ya CCM ukiibuliwa na wabunge wa upinzani na hii ilikua sasa ni mila na desturi zetu Watanzania.
Kumbe kulikua na namna, wanaccm wanaibuwa uchafu, wanampa Mbunge wa upinzani wampendae na pindi kitanuka basi jamaa atalipwa credit.
Na kila siku scenario ilikua ni ile ile. Wapinzani wanaibuwa madudu, Serikali kuu inakanusha na kukataa, mwisho wa siku mambo yanawekwa hadharani, Serikali inakiri, tume inaundwa, baadhi ya mawaziri wanapoteza nafasi zao.
- Mfano : Buzwagi, Richmond, Tegeta Escrow account.
Hii ikamfanya mbunge wa upinzani Zitto kujiona ana ujasiri, kujiamini na kupata sifa na imani kubwa toka kwa Watanzania.
Lakini ukichunguza kwa undani, utakuta Zitto hakua anajua lolote tofauti na kutumika kwa kulipwa ganji kidogo.
Watanzania wengi wakajaribu kufikiri kwamba Zitto hawezi kukosea, wala kudanganya, na anajua kila kitu maana kila anacho ibuwa kinakuwa ni cha kweli.
Zitto baada ya kulewa misifa na wakati anatumika kwa ganji, akajisahau kabisa na kujiona kinara, na mtu asiekuwa wa kawaida kabisa ( 2008-2015).
Kuanzia 2015, akaja rais ambae ni mkali, mzalendo, hataki kusikia upuuzi, msimamizi mkali wa rasilimali za Watanzania, adui wa Rushwa na mafisadi ambae ni Dkt. John Joseph Pombe MAGUFULI.
Agenda za wapinzani zote zikahamia CCM tena kwa utekelezaji madhubuti.
Wapinzani wengi wakaanza kuvutiwa na utendaji kazi wa Mhe. Rais John Joseph Pombe MAGUFULI.
Ilifikia stage vyama vya Chadema na ACT Wazalendo wakijinadi kwamba mhe.Rais anatekeleza ilani yao na ndomaana anakwenda vizuri na wakati wamesusia na kutoka nje kipindi anazindua bunge.
Wengi tukajua sasa viongozi wa upinzani wengi na hasa Zitto kabwe watampenda sana Rais MAGUFULI kwakua anatekeleza yale waliokua wakipigania toka miaka ya 2005.
Kumbe viongozi Hawa wa upinzani wakalichukulia kama changamoto kubwa litakalo wanyima fursa za kuibuwa tena madudu, kujijengea umarufu kwa wananchi kama walivyo zoea.
Mianya na vyanzo vyote vya uvujishaji wa taarifa za Serikali vikafungwa, wapinzani hawapati tena taarifa nyeti na Serikali inakuwa makini kuchukua hatua Kali kabla hata ya uchafu kutokea na
wale rafiki zake Zitto wakawa nje ya ulingo.
Kwa Zitto ikawa tabu sana maana kazoea siasa za sifa na kuibuwa madudu ya Serikali na kulipwa chochote kitu kila mara. Sasa mfuko umetoboka.
Wananchi nao na washabiki wake wakawa sasa wanasubiria chochote kitu ( Taarifa nyeti) toka kwa Zitto bila mafanikio. Sifa na imani vikaanza kupungua.
Kwanza kabaki pekeake, wengine wamesha hamia CCM, mifereji ya kuvujisha taarifa nyeti imesha ziba.
Hapa sasa Zitto anaanza kuzisaka taarifa kwa vyanzo vingine tofauti ambavyo havina uwezo wakupata taarifa nyeti.
Ndomaana kwasasa anakua anatoa vijitaarifa visivyokua na ukweli, vyenye kuonyesha chuki binafsi dhidi ya mhe. Rais ili kuwaonyesha wananchi kwamba bado yupo vizuri.
Wananchi bado wakiwa na concept yao ile ile ya zamani ya kufikiri kua Zitto ni mbunge mahiri, anajua kila kitu, na Serikali ya CCM ni ile ile yenye tabia za kukataa taarifa kwanza then kuja kukubali baadae.
Kwasisi tuliofanya kazi na Zitto kwa mda, tunamjua nje, ndani ( in and out), tunajua fika kua yupo frustrated kwa kuona sifa na imani kwa wananchi vikizidi kupungua siku hadi siku.
Anachokifanya kwasasa ni kuongea kila kitu kama Kasuku bila utafiti ilimradi apate political sympathy na kiki toka kwa wananchi.
Na simshangai hata kidogo maana yupo pabaya kwasasa, jimbo la Kigoma mjini na Manispaa ya Kigoma ujiji vinaenda kupotea 2020, kwenye kugombea urais hawezi kushinda hata atambikie ziwani Tanganyika.
Kinachompa tabu ni baada ya 2020, atakua nani? Je imani na sifa zake kwa Watanzania vitapanda au kufa kabisa?
Anatia Huruma eehhhh,
CWU tiz.