Tarehe kama ya leo mwaka 2018 niliandika makala ktk huu ukurasa wangu iliyokuwa na kichwa kilichosemeka kuwa 'JE UNA LA KUJIFUNZA KWA 'CURVEBALL' WA IRAQ?'
Katika makala hiyo niliangazia mbinu ambazo Marekani na mshirika wake Uingereza walizozitumia ili kupata uhalali wa macho ya kimataifa wa kulivamia kijeshi taifa la Iraq. Mpaka leo imethibitishwa mara kadhaa kuwa sababu zilizotolewa na Marekani kuhusu uwepo wa silaha za kemikali nchini Iraq hazikuwa sababu za kweli, japo watu wengi walipoteza maisha kwa risasi, njaa na magonjwa kutokana na uvamizi ule, mpaka leo Mashariki ya kati haijatulia kutokana na makovu ya ule uvamizi.
Fuata viunganishi hivi kusoma zaidi:
- https://en.wikipedia.org/wiki/Curveball_(informant)
- https://www.nytimes.com/2011/02/16/world/middleeast/16curveball.html
- https://www.telegraph.co.uk/news/worldnews/middleeast/iraq/8326344/Iraqi-defector-Curveball-admits-WMD-lies.html
- http://www.nbcnews.com/id/41609536/ns/world_news-mideast_n_africa/t/curveball-i-lied-about-wmd-hasten-iraq-war/#.XHYleIgzbIU
- https://www.independent.co.uk/news/world/politics/man-whose-wmd-lies-led-to-100000-deaths-confesses-all-7606236.html
Kwakuwa andiko hili ni refu kidogo, niwashauri wale wasiokuwa na uwezo wa kusoma waachane nalo maana hutaelewa kitu na badala yake unaweza kuishia kutukana baada ya kushindwa cha kukoment. Katika andiko andiko hilo la tarehe 25 Februari 2018 niliandika yafuatayo.
__________________________ _________
Rafid Ahmed Alwan al-Janabi, ambaye vyombo vya usalama vya Marekani na Ujerumani vilimpa jina la kificho la Curveball ndiye mtu ambaye alitumika kwa kiasi kikubwa kuithibitishia Marekani na kuharalisha propaganda za Marekani kuwa Sadam Hussein anamiliki silaha za Nyuklia. Ukitafuta neno Curveball ktk 'search engine' yoyote utaweza kujifunza mengi kuhusu uongo uliosababisha uvamizi na vifo vya wairaq zaidi ya 100,000 mpaka sasa na bado hali ni tete.
Marekani ilitaka mtu ambaye anaweza kuthibitisha madai yao ili wapate sababu za wazi za kuishambulia Iraq, kwahiyo alipojitokeza Rafid ikawa Mungu amejibu maombi ya Marekani. Baadhi ya taarifa zinasema Rafid alitumiwa na vyama vya upinzani na makundi ya watu ambao walikuwa wakitaka Sadam Hussein aangushwe kwa gharama yoyote ile ktk kushirikiana na Marekani na Uingereza ili kuwezesha uvamizi utakaoweza kumuondoa Sadam madarakani.
Taarifa zinasema kuwa Rafid almaarufu kama Curveball ndiye 'Spy' aliyefanikiwa kuvidanganya vyombo vya ulinzi na usalama mbalimbali duniani kwa mafanikio makubwa. Lakini, wengine wanasema japo mataifa ya Marekani na Uingereza walitilia mashaka taarifa za Rafid, hawakutaka kupoteza muda maana walikuwa wamepata mwanya salama na safi kutekeleza malengo yao ya uvamizi.
Mwaka 1999 ndipo Rafid alipowasili ktk kambi ya wakimbizi ya Ujerumani na kuomba hifadhi, hapo ndipo alipoanza kuwalisha uongo uliofanana na kweli. Rafid alipohojiwa alisema kjwa "“I had the chance to fabricate something to topple the regime. I and my sons are proud of that, and we are proud that we were the reason to give Iraq the margin of democracy.”--Rafid Ahmed Alwan al-Janabi aka CURVEBALL
Kwa tafsiri isiyo rasmi" nilipata nafasi adhimu ya kutengeneza uongo unaoweza kuuangusha utawala wa kipindi hicho (Sadam Hussein), mimi na mwanangu tunajivunia hilo, na tunajivuna kwa kuwa sababu/sehemu iliyoipa Iraq utawala wa kidemokrasi "
Kwa kauli hii ya Curveball na kauli zake. nyingine nyingi unaweza kuona kuwa huenda Sadam Hussein alichukiwa na baadhi ya watu kiasi kwamba sababu yoyote hata ikiwa haramu inayoweza kumuangusha Sadam ilionekana baraka na nzuri bila kujali madhara yake.
Wakati makundi yanayompinga Sadam pamoja na vyama vya upinzani vikimtumia Rafid ili atoe taarifa za uongo kuhusu Iraq, Marekani pia ilikuwa ikisubilia kwa hamu taarifa hiyo ya uongo ya Rafid ili waitumie kuharalisha mpango wao wa kuivamia Iraq kwa maslahi yao binafsi.
Mashirika ya kimataifa, vyama vya siasa,. makundi ya kijamii na wanaharakati wa dini waliisaidia Marekani na Uingereza kuuaminisha umma kuwa Sadam Hussein alikuwa akizalisha silaha za maangamizi/Nyukilia (Nuclear Weapons).
Propaganda zisipopingwa kwa nguvu zote, kuna ambao huziamini na kuziabudu propaganda hizo. Idadi ya watu walioziamini propaganda zao iliendelea kukua kila siku, mpaka Marekani na Uingereza walipofanikiwa kuivamia Iraq na kuhakikisha kuwa Sadam Hussein ananyongwa.
Lengo kuu la kuivamia Iraq ilikuwa kuhakikisha kuwa wanamzuia Sadam Hussein ktk kuzalisha silaha za maangamizi ambazo kwa mujibu wa Marekani walisema zipo silaha za maangamizi zilizotengenezwa zinazotishia dunia hususani mashariki ya kati. IKIWA suala la Silaha za Nyuklia ndiyo sababu kuu, ulimwengu haukutegemea pasiwepo tena na silaha za nyuklia huku wahusika wakianza kubainika kuwa walijipikia hiyo sababu ilimradi Sadam aondolewe. Hii inatoa tafsiri ya kuwa, lengo kuu ni Sadam kuondoka bila kujali kama sababu inayosemwa ina mashiko au haina, lakini kwanza atoke hilo tunalijua leo.
Walitumia kila mbinu ktk kuuthibitishia umma wa Iraq na ulimwengu kuwa Iraq ina silaha za Nyuklia hivyo ni tishio kubwa. Lakini baada ya uvamizi kitu cha kwanza Marekani na wenzake kukidhibiti ilikuwa wizara ya mafuta, visima vya mafuta na miundombinu ya mafuta, na mpaka leo hii Marekani ina ushawishi mkubwa sana ktk nyanja hizo nchini Iraq.
Aliyekuwa Waziri wa ulinzi wa wakati huo, Collins Powell aliliambia bunge la seneti kuwa Iraq ilikuwa na silaha za Kinyuklia ambazo ni hatari, Powell alisema kuwa Rafid ambaye alikuwa ni Chemical Engineer ktk kile. kilichoitwa kuwa ni mpango wa Sadam wa kutengeneza silaha za nyuklia alikuwa na ushahidi wote na hata ushahidi kwamba watu zaidi 13 walikufa ktk moja ya vituo vya kinyuklia huko Iraq wakiwa ktk utekelezaji wa mpango huo wa kuzalisha silaha za nyuklia. Marekani dhidi ya Iraq.
Rafid aliyetumika kufanya propaganda za kuuaminisha umma kuwa kuna silaha za nyuklia Iraq baadae aikuja kukiri kuwa hakukuwa na kitu kama hicho na kwamba eti. alidanganya ili tu Sadam angolewe madarakani. Hata hivyo waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani, Donald Rumsfeld alikwishatanabahisha kuwa Iraq haikuwa na silaha za kinyuklia.
Neno moja la. uongo la Rafid Janabi. liliipa sababu Marekani kugeuza Iraq kjwa uwanja wa vita, inakadiriwa kuwa watu zaidi ya 100,000 wamepoteza maisha tangu Marekani ilipoivamia Iraq. Makovu ya uvamizi huo yamesababisha makundi ya kiasi kuongezeka na yale yaliyokuwepk yalipata mwnya wa kupevuka na 'kunawili' mpaka leo hii ikazaliwa Isis na mengineyo, hakuna uthibiti wa serikali kwa asilimia 100 ya taifa la Iraq, kila kundi la waasi linathibiti sehemu yake huku serikali nayo ikipambana kujiimarisha bila mafanikio. Je nani ananufaika na hilo hali??
Rafid alipohojiwa na gazeti la The Times na The Guardian alikiri wazi kuwa yeye alidanganya ilimradi ipatikane sababu itakayowezesha Sadam kuondoka au kuondolewa madarakani kwa namna yoyote ile. Rafid hakujali kuwa wanaotaka kumuonfoa Sadam madarakani wanafanya hivyo kwa sababu ya ajenda zao binafsi, yeye hakujali ajenda za Marekani waka Uingereza, yeye. na wenzake wa upinzani walitaka Sadam atoke na alitoka.
Je silaha za maangamizi za kinyuklia ambazo walisema zinazalishwa Iraq ziliwahi kupatikana? Baada ya uvamizi ndipo ripoti mbalimbali zinathibitisha kuwa hakukuwa na silaha za maangamizi Iraq bali ilikuwa propaganda tu.
Lakini walifanikiwa kuwatumia wairaq, mashirika, vyama vya upinzani, taasisi mbalimbali za dini kuhakikisha kuwa adui namba wa Iraq anakuwa Sadam Hussein kabla hawajavamia. Wairaq waliisaidia Marekani na Uingereza kuivamia Iraq leo wanajuta, maisha ya Iraq baada ya kuuliwa kwa Sadam Hussein ni hatari tupu zaidi ya kipindi cha Sadam Hussein.
Sipingi matendo maovu yaliyokuwa yakiripotiwa mara kwa mara kuhusu Sadam na utawala wake bali mimi nahoji sababu iliyoitwa ya MSINGI ( uwepo wa silaha za maangamizi) iliyotumika kuharalisha uvamizi dhidi ya Iraq na kupelekea vifo vya maelfu na vurugu zizisokoma, sababu ambayo mpaka imegundulika ilikuwa 'fake intel' .
Huenda Sadam hakutakiwa kuendelea kuwa Rais wa Iraq kwa mujibu wa wapinzani wake wa ndani na nje huenda Sadam alikuwa dicteta asiyefaa na kwamba ilikuwa ni sawa kabisa kumuondoa madarakani lakini sababu iliyotolewa ktk uso wa dunia kuwa Iraq ina silaha za kinyuklia na sababu hiyo ndiyo ikatumika kuivamia Iraq HAIKUWA YA KWELI.
Walijua wakitumia sababu ya kweli kwamba hawamtaki Sadam Hussein kwasababu anaziba maslahi ya Marekani au Uingereza ktk mafuta nk wananchi hawawezi hata siku moja kuunga mkono hata kama Sadam Hussein alikuwa dicteta. Propaganda kuhusu silaha za Nyuklia zilifanywa kwa ustadi wa hali ya juu sana, wananchi waliambiwa kuwa Sadam akifanikiwa kutengeneza silaha za nyuklia atazitumia dhidi ya wapinzani wake wa ndani ya nchi, kauli za aina hiyo ziliwaunganisha wapinzani dhidi ya serikali na Sadam kwa kuamini kuwa Sadam ni kifo chao cha kesho. Hakuna aliyetaka kuhoji kuwa Marekani au Uingereza leo wanatuonea huruma bure? Haya mapenzi ya Marekani yameanza lini na taifa hili la kiarabu??!
Kwanini waliamua kutumia sababu ya uongo ili tu wafanikiwe kupata kibali ktk macho ya kimataifa cha kuivamia Iraq? Kwanini hawakutafuta sababu yenye ukweli ili hata baada ya miaka 100 historia isije kutambua kuwa kuna mahala watu mataifa au makundi flani yaliungana kufanya tukia kwa kutumia sababu za kupika? Hata wakitumia uongo,. ilimradi ktk kipindi cha wakati huo utaonekana kuwa ni ukweli, wakimaliza lengo lao hakuna kitakachobadilisha yatakayotokea ktk vuta au hayo malengo yao hata kama ni miaka mingapi ijayo. Hiroshima na Nagasaki yalipigwa mabomu ya atomic kwasababu zao lakini walijificha ktk vita ilihali yalikuwa majaribio lakini mpaka leo ni vilio.
Magoiga SN|¦| Think Beyond The Obvious