Watu wengi hawaelewi kisa cha wabunge wengi wa upinzani hasa cdm kupagawa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi. Hofu yao kubwa ni kasi ya utendaji wa jpm ambaye amejizolea sifa na kukifanya chama cha mapinduzi kukubalika tena baada ya kukirejesha kwa kiasi kikubwa kwenye maadili sera na itikadi yake. Wabunge na viongozi wa upinzani wanajua ni vigumu kuchaguliwa mbele ya ccm kwa kazi nzuri inayofanywa na serikali yao hivyo wameweka mkakati wa kugeuza kila jema la serikali ya ccm kua ujinga na kichekesho. Wanaamini wakirudia rudia kila siku kubeza kila zuri hatimae watu wataamini na kuichukia ccm na jpm.
Watu kama zitto na halima mdee hawajawahi fanya kazi nyingine zaidi ya ubunge. Kwa ubunge wametajirika na wana mali nyingi. Hawajui kazi ya kufanya baada ya ubunge. Aheri watu kama sugu na prof jay wanaweza kurudi kwenye bongo fleva kwa shingo upande.
Wapinzani wa aina ya cdm na zitto ndio wanaitwa wapinga maendeleo 'reactionaries'. Kwa aina ya upinzani uliopo nchi haifaidiki lolote na upinzani na inaweza isisonge mbele. Wapinzani katika nchi yetu saa zote wanaiombea nchi balaa na majanga. Wanaomba serikali ikwame. Wanazusha uongo na kuichimbia mkwara ili wapate cha kusema.
Hebu fikiri mtu anajaribu kuaminisha watu serikali kununua ndege kwa kulifufua shirika la taifa la ndege ni jambo la ujinga mkubwa bila ya kuweza kutoa sababu kupinga hoja za serikali. Mtu anawaambia watu tena kwa jazba kujenga reli au kujenga bwawa la steagler gourge kupata umeme mkubwa ni ujinga huku hana sababu ya maana.
Hawa yafaa kuwaondoa kwenye ulingo wa siasa nchini wasije tuletee balaa.