Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amempongeza Mkandarasi anayejenga Soko kuu la Morogoro mradi unaojengwa kupitia fedha za Serikali za miradi mikakati katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mkandarasi huyo mzawa aitwaye Nandra Engineeeing ameonyesha uwezo mkubwa na umakini katika kazi yake.
Soko kuu la Morogoro ni mradi mkubwa unao fadhiliwa kwa fedha za Serikali utakao gharimu jumla ya shilingi bilioni 17.
Ziara ya kikazi ya Waziri Jafo imekamilika kwa kutembelea mikoa miwili ya Pwani na Morogoro ambapo alifanikiwa kutembelea shule ya sekondari Maneromango, Shule ya Sekondari Kilakala, Ujenzi wa Soko kuu Manispaa ya Morogoro pamoja na ujenzi wa shule ya Sekondari Mji Mpya inayojengwa na Vikosi vya ujenzi kwa kutumia utaratibu wa Force Account.