CHACHA WANGWE NA UENYEKITI CHADEMA 2008
Mwaka 2008 ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kulikua na vuguvugu na joto kali la uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa na mmoja wapo wa watu waliojitokeza hadharani kutaka kugombea nafasi hiyo si mwingine bali alikua ni Mbunge machachali na mwana siasa mwiba kutoka Tarime ndugu Marehemu Chacha Zakayo Wangwe ambae alikua ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA alijitokeza wazi wazi kutaka kuwania nafasi hiyo ya uongozi wa juu akiainisha mapungufu na madhaifu mbali mbali ndani ya CHADEMA chini ya uongozi wa Mh.Freeman Aikael Mbowe mapungufu hayo yalimskuma akatoa WARAKA WA CHACHA WANGWE KWA CHADEMA na baadhi ya mapungufu hayo ni kama yafuatayo;
1.Matumizi mabaya ya ruzuku ya chama
2.Madeni ya uchaguzi (Mwenyekiti kukikopesha chama bila makubaliano na vikao halali vya chama)
3.Uteuzi wa upendeleo wa wabunge wa viti maalum
4.Utendaji wa kibabe
Baada ya mnyukano mkali na kuona kuna kupoteza nafasi ya uenyekiti Mh.Chacha Wangwe aliundiwa zengwe ya kusimamishwa uongozi na kukutana na kadhia ya kufukuzwa uanachama na kamati kuu iliyoongozwa na mbowe wakihofia ushawishi na kujiamini kwa hali ya juu aliyokua nayo Wangwe hivyo baada ya kikao hicho kuvuliwa uongozi Wangwe aliamua kutoka Dodoma kurejea Dar es salaam ambapo akiwa njiani siku ya Tar 30/07/2008 alipata ajari mbaya ya gari na kufariki hapo hapo lakini DREVA WA CHACHA WANGWE ALIPONA huo ukawa mwisho wa ndoto za Chacha Wangwe kuupata UENYEKITI WA CHADEMA TAIFA . Baada ya kifo chake uchaguzi uliifanyika na Freeman Aikael Mbowe alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
Pitia waraka wa Chacha Wangwe.
WARAKA WA CHACHA WANGWE KWA CHADEMA,ALIUANDIKA SIKU CHACHE KABLA YA KUFAA - HAKI LEO
chacha2-jpg.596036
Ajari iliyotoa uhai wa CHACHA WANGWE na DREVA WAKE AKITOKA MZIMA mpaka leo yupo Hai
ZITTO ZUBER KABWE NA UENYEKITI WA CHADEMA TAIFA
Mwaka 2013 tuliona vuguvugu la kutaka kubadilisha uongozi wa CHADEMA Taifa kwa Naibu Katibu Mkuu Bara ndugu Zitto Zuber Kabwe kuja na mkakati wa mabadiliko ndani ya Chacha alianza kuunda team yake ya kuweza kumsaidia kufikia adhima yake hiyo aliunda team yake ya ushindi na katika team hiyo alikuwepo Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha Samson Mwigamba,alikuwepo mjumbe wa Kamati kuu CHADEMA Prof.Kitila Mkumbo na safu hii ilikuja na naandiko likiitwa MKAKATI WA MABADILIKO katika andiko hili waliorodhesha mapungufu na madhaifu yaliyopo ndani ya chama na nini kiifanyike ili kuweza kuyatatua,kama ilivyo kwa CHACHA WANGWE nao pia walianisha mapungufu yaliyopo ndani ya CHADEMA ni kama ifuatavyo
1.Matumizi ya fedha yasiyofuata taratibu ndani ya chama
2.Nafasi za upendeleo ndani ya chama
3.Kukopesha chama bila kufuata taratibu
4.Njia haram za kubaki madarakani
Mkakati huu ulivuja ndani ya Chama hivyo ikapelekea Samson Mwigamba na Kitila Mkumbo kuvuliwa uanachama wao ndani ya CHADEMA huku Zitto Kbwe mwaka 2013 akivuliwa nyazifa zote za uongozi ndani ya CHADEMA hali hii ilifanya Zitto aendelee kupigan ndani ya chama na katika vita hii Zitto Kbwe alivuliwa rasmi uanachama wa CHADEMA March 2015 ndipo alipokiimbilia mahakamani na kwa kuendeleza kile Zitto aliikiamini walirushiana maneno na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Aikael Mbowe na katika vita hiyo ya maneno Zitto alinukuliwa na Gazeti la Raia Tanzania na maneno hayo akimlenga Mbowe
"CHACHA WANGWE DIED I WONT"
Swali la kujiuliza kwa nn Zitto atamke maneno hayo na alikua akimlenga nani hasa kwani Zitto alivuliwa uanachama wakati wa vita ya uenyekiti na Wangwe nae alifariki wakati wa harakati za kugombea uenyekiti ndani ya CHADEMA na katika vita hiyo ya Wangwe na Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Taifa alishinda Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Taifa na Wangwe alifariki pia katika vita ya uenyekiti kati ya Zitto na Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Taifa hapa Zitto alifukuzwa uanachama na Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Taifa akashinda uenyekiti?Hapa kuna swali la kujiuliza na la kufanyia kazi. Pitia link hapo chini kupata habar kamili ya Zitoo kusema HATOKUFA KAMA ALIVYOKUFA CHACHA WANGWE
Zitto aanika siri nyeti za Mbowe! Adai hatakufa kama Chacha Wangwe...
KUIBUKA KWA TUNDU LISSU KAMA MWANA SIASA MACHACHARI KUELEKEA UCHAGUZI WA UENYEKITI WA CHADEMA TAIFA OCTOBER 2018.
Katika siku za hivi karibuni hakuna mwananchi na mtanzania asiyekubali kuwa Tundu Antipas Lissu alikua aking'ara kwa kishindo na akionekana kuwa ni mwana siasa machachali kutoka upinzani,ni katika kipindi hiki Tundu Lissu alikua ana wika kwa kiwango cha juu na alikua akisikka zaidi katika siasa za upinzani kuliko mtu yeyote katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa CHADEMA Taifa tunaona ni Tundu Lissu aliyekua na mvuto na anavutia vijana wengi kuliko mwana sasa yeyote katika kambi ya upinzani sio siri Lissu alikua akisikika kuliko Katibu Mkuu wa CHADEMA,Lissu alikua akisikika sana kulko Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Lissu alikua akisikika zaidi ya Katibu Mkuu CHADEMA bara na CHADEMA Zanzibar hivyo kuwa mwana siasa aliyepo katika maskio na midomoni mwa wana CHADEMA na wana upinzani kwa ujumla
Hali hii inawafanya na iliwafanya watu wengi waamini ndio mtu pekee anayeweza kutiikisa na kukijenga CHADEMA kama akipewa nafasi ya uenyekiti Taifa CHADEMA kwani mtu pekee mwenye ujasiri,uthubutu na kujiamini hivyo watu wengi walianza kumsema kuwa anafaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mwaka 2018.
Lakini hilo halikutokea kwani mwaka mmoja kabla ya uchaguzi huo September 06,2017 Mwana siasa huyu mashuhuri alivamiwa nyumbani kwake na kupigwa risasi akiwa katiika gari lake mpaka sasa yupo hoi hospiatal nchini Kenya kwa matibabu na katika hali ya kushangaza dreva wake alitoka salama salmini bila kuwa na jeraha lolote na kinachoongofya zaidi dreva huyo alihojiiwa na gazeti la Mwananchi alisema hana kumbukumbu sawa kwa tukio la kuvamiwa kwa Lissu wakati hapo awali alinukuliwa na gazeti la mwana halisi akielezea tukio zima mpaka kutaja namba ya gari na ana ya gari la watu waliowashambulia habari hiyo iko katika link hapa chini
Dereva wa Lissu asema hana kumbukumbu vizuri kwa kilichotokea kwenye shambulio dhidi ya Lissu
MASWALI YA KUJIULIZA.
1.Kwa nini kila anayejitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA anayeonekana ni tishia huvuliwa uongozi au kufukuzwa uanachama?Nafasi ya uenyekiti wa chama hiki una nini?
2.Katika vita ya maneno ya Zitto na Mwenyekiti huyo kwa nini Zitto aseme ''CHACHA WANGE DIED I WONT'' hii kauli ina maanisha nini?Kuna nini nyuma ya pazia juu ya Kifo cha Chcha Wangwe mpaka Zitto atoe kauli hii?
3.Katika harakati za kuutaka uenyekiti Chacha Wangwe alipata ajari akafarikii dunia na dreva wake akatoka salama salmini na katika nyakati hizi tukielekea uchaguzi wa chama 2018 Lissu akiiwa katika pick ya hali ya juu anashambuliwa kwa risasi zaidi ya 25 yeye anapatwa na maeraha makubwa lakin dreva wake anatoka salama salmin na katika kutoka huko anaelezea tukio zima kisha anaenda Nairobi kwa matibabu ya kisaikolojia alivyoanza kupata tu matibabu hayo anaanza kupoteza kumbukumbu juu ya tukio zima kuna nini nyuma ya pazia?Na matibabu hayo ya kisaikolojia nani anaya gharamikia?
Kuna msemo wa wahenga wanasema "ANAYELIA SANA MSIBANI HUYO NDIO MCHAWI"
Wasalaam