Utawala wa sheria, Uhuru wa kuongea na mipaka yake, Kwako Jenerali Ulimwengu - Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

"Muda Unaongea"

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

27 Feb 2019

Utawala wa sheria, Uhuru wa kuongea na mipaka yake, Kwako Jenerali Ulimwengu


Ninachotaka kusema ni kuwa duniani kote jamii na taifa hujiwekea utaratibu wa kisheria na kikanuni wa kuwaongoza ktk masuala mbalimbali. Inaweza kuwa ktk ulinzi na usalama, rasilimali madini, uoto wa asili, tamaduni na mila, familia, ndoa, kazi, ustawi wa jamii nk.
Image may contain: 1 person, closeup
Lakini pia, jamii hujitengenezea utaratibu mpya wa kuwaongoza kwa kutegemea na mabadiliko au mahitaji mapya ktk jamii husika. JUZI nimemsikia mzee wangu JENERALI ULIMWENGU akisema maneno yafuatayo,

“Mtu yeyote anayewakataza watu kuzungumza jambo Fulani anatengeneza mazingira ya uasi, hivyo ni muhimu watu waachwe huru kuzungumza” Jenerali Ulimwengu.

Sipingani na nukuu ya mzee wangu Jenerali Ulimwengu, japo ningefurahi sana iwapo Jenerali akiwa ni mwanasheria na mwandishi mkongwe asaidie kukumbusha kuwa uhuru wa kuongea unayo mipaka yake kikatiba, kisheria na hata kikanuni. Uhuru wa kuongea haupaswi kuvunja sheria au kuingilia haki za wengine, yaani huwezi kunitukana au kunichafua kwasababu tu ni uhuru wako wa kuongea, ndiyo maana sheria imetoa nafasi iwapo nimeona kuwa umeingilia haki yangu niende mahakamani kuomba tafsiri au kudai fidia ya kulinda utu na heshima yangu. Kwahiyo haki ya kuongea haikupi kinga kuvunja sheria au kuingilia haki za wengine.

Sidhani kama Tanzania watu wanazuiliwa kusema mambo flani flani, hakuna mtu aliyewahi kuzuiliwa asiongee Tanzania, ila ninachokiona kwa muda mrefu ni kuwa watu wakitumia haki yao ya kuongea hawataki wengine waende mahakamani kulalamika au kuomba tafsiri ya kauli walizozitoa. Yaani hapa nchini, watu wanataka wakiongea jambo asitoke wa kwenda mahakamani kulalamika au kutafuta haki yake iwapo anaona kuna mtu ameiingilia. 

Kila mwananchi anao wajibu wa kufuata utaratibu wa nchi husika, na kulinda katiba, sheria na kanuni za nchi husika. Iwapo kwa hisia zako, au kwa tafsiri ya mamlaka yoyote ndani ya nchi ikiona kuwa mtu flani amekosea au amekiuka taratibu flani flani, mahala sahihi pa kuamua utata huo au mvutano huo ni mahakamani na siyo vinginevyo. 

Naomba ifahamike kuwa, uhuru wa kuongea na uhuru wa mawazo ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi, na nchi nyingi duniani zimeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolinda uhuru wa mawazo na uhuru wa kuongea. Kinachofanyika kote duniani ni kuwa, nchi hutunga sheria na kanuni mbalimbali zinazowaongoza wananchi ktk masuala mbalimbali, hivyo pamoja na kwamba unaweza kuwa una uhuru wa kuongea lakini haupaswi kuvunja sheria nyingine au kuingilia uhuru wa wengine. 

Kwahiyo, mtu anaweza kutoa mawazo yake au anaweza kuongea chochote maana ni haki yake ya kikatiba, lakini iwapo yeyote ataona kuwa haki zake zimeingiliwa au amedhihakiwa au utu wake na heshima yake imevunjwa mahala pekee pa kuweza kwenda kulalamika ni ktk mahakama kama chombo cha kisheria. 

Mtu au taasisi inaenda mahakamani kuhoji uhalali wa maneno yaliyosemwa na mtu ili apate haki yake, au apate tafsiri ya maneno yaliyosemwa dhidi yake iwapo hayakiuki haki yake, utu wake, heshima yake au hayavunji sheria. 

Alichokisema Halima Mdee ametumia haki yake ya kikatiba na kisheria, na walimpeleka mahakamani nao wametumia haki yao kikatiba na kisheria ili waweze kujiridhisha kuwa haki zao hazijavunjwa na Halima wakati alipokuwa akitumia haki yake ya kuongea na kutoa mawazo yake.

Mwisho wa siku mahakama ndiyo itakayoamua iwapo Mdee alikuwa sawa, yaani hajavunja sheria au hajaingilia haki za wengine au lah. Kwasababu mahakama inafanya kazi kwa uhuru na weledi, hukumu au maamuzi ya makahama kwa kiasi kikubwa huzingatia ushahidi usiokuwa na mashaka, na nikirejea ile kauli aliyoitoa Halima Mdee siku za karibuni kuhusu Ndege, kwakuwa sasa limefika ktk chombo cha haki, hapo ndipo tutajua iwapo Mdee alikosea ktk macho ya kisheria au alikuwa sawa ktk muktadha wa kuvunja sheria au kuingilia uhuru wa wengine. 

Huo ndiyo utawala wa kisheria unavyotakiwa kuwa kokote duniani, na ndivyo ilivyo hata Tanzania. 

Post Bottom Ad