Sheria ni nmsumeno, siyo machozi yetu - Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

"Muda Unaongea"

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

24 Feb 2019

Sheria ni nmsumeno, siyo machozi yetu


Hukumu iliyotolewa leo na Mahakama ya Kisutu ambayo imewahukumu kifungo cha maisha jela watu nane, kwa kosa la kuchoma moto Kituo cha Polisi Bunju A mwaka 2015, ni hukumu ambayo inahuzunisha kutokana na historia ya tukio lenyewe lililopelekea vurugu, mpaka kuchomwa moto kwa kituo hicho.


Pamoja na huzuni hizo, bado ukweli unabaki palepale kuwa watuhumiwa wamepatikana na hatia kwa mujibu wa sheria na wamehukumiwa kwa mujibu wa sheria zetu. Kesi hiyo ilikuwa ikiwakabili washtakiwa 35, ambapo awali 17 waliachiwa huru, na kati ya 18 waliobaki, 8 ndio wametiwa hatiani, na 10 wameachiwa huru leo. 

Ukisoma sura ya thelathini na tano, makosa yanayosababisha uharibifu wa mali, Uchomaji wa mali kwa makusudi Sheria Na. 2 ya mwaka 1972, 319.

Mtu yeyote ambaye, kwa kunuwia na isivyokuwa halali anatia moto katika– 
(a) Jengo lolote lile liwe limekamilika au bado ; au 
(b) chombo chochote kile kiwe kimekamilika au bado; au 
(c) lundiko lolote la mazao ya mboga, au la makaa ya mawe, madini au la kuni; au 
(d) viwanda vya machimbo au matengenezo au zana za machimbo ya madini atakuwa anatenda kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha.

Hawa vijana walifunga barabara kuishinikiza serikali kuweka matuta ktk eneo ambalo wanafunzi wenzao walikuwa wakigongwa na magari kila kukicha, sababu yao ilikuwa ya msingi na dhamira yao ilikuwa njema,lakini bado waswahili husema sheria ni msumeno. Japo watuhumiwa wengine walikuwa na umri mdogo wakati wanakamatwa mwaka 2015, bado hiyo haiwezi kuwa utetezi kwamba wasihukumiwe iwapo mahakama imejiridhisha kwa ushahidi uliowakilishwa pasipo na shaka. 

Katika dhana ya uhuru wa Mahakama, naweza kusema mahakama iko sahihi ktk hukumu yake kutegemea na ushahidi uliowasilishwa, na sasa ni wajibu na haki ya wahusika kukata rufaa iwapo wanazosababu zinazoweza kubatilisha hukumu iliyotolewa leo, huo ndiyo utaratibu wa kimahakama na wala siyo kwa kutegemea hisia za kila mmoja wetu analitafsiri vipi chanzo au tukio lililopelekea kuchomwa moto kwa kituo hicho cha polisi. 

Hukumu inatolewa kwa kutegemea na mwongozo wa sheria na kanuni za adhabu, iwapo itathibitika pasipo na shaka kulingana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani, na wala siyo kiwango cha machozi wanayoyatoa watuhumiwa au ndugu wa watuhumiwa. 

Kwa ushauri wangu, ni vyema wahusika wakate rufaa kama hawakubaliani na hukumu hii iloyotolewa leo, maana ndiyo njia pekee ya kukwepa kifungo hicho iwapo wataona wanaweza kuishawishi mahakama kuwapunguzia kifungu na siyo machozi pekee.

Binafsi nitaendelea kuamini kuwa mahakama imetenda haki, maana hizi adhabu huwa ni 'written' na siyo kwamba zinatoka mfukoni mwa hakimu. Cha msingi tuendelee kuwaombea hawa ndugu zetu ili wapate nguvu za kuendelea kukata rufaa na kama rufaa wakishindwa basi tuwaombee Mungu awape wepesi wa kutumia adhabu yao.

Nitashnagaa sana watu ambao miaka yote wanapigania mahakama isiingiliwe wakiwa mstari wa mbele kukosoa hukumu ya mahakama kwa machozi au msikitiko yao na kusahau kuwashauri au hata kuwawezesha wahusika wakate rufaa. 

Post Bottom Ad