Muujiza wa Zitto Kabwe Ulaya, Mtangazaji wa DW amkaba koo - Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

"Muda Unaongea"

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

24 Feb 2019

Muujiza wa Zitto Kabwe Ulaya, Mtangazaji wa DW amkaba koo

Dr Yahya Msangi Anaandika Kuhusu MIUJIZA YA WAPINZANI
Nimemsikiliza Zitto Zuberi Kabwe (King Mawese) akihojiwa na DW Mjini Bonn alikokuwa akihudhuria mkutano wa Chama rafiki na ACT. Alieleza kuwa Chama hicho kinategemea kupata takriban wabunge 7 katika Bunge la EU. Mtangazaji akamuuliza ni manufaa yapi ambayo Tanzania itayapata kutokana na yeye kuhudhuria kikao hicho na Chama hicho rafiki kupata viti kwenye Bunge la EU?. Hapo ndipo maajabu ya wapinzani nchini Tanzania yalipojidhihirisha.

Kwa kujiamini kabisa Zitto akasema kuwa amewasilisha maoni ya ACT ambayo Chama rafiki kitayawasilisha Bunge la EU kikipata viti. Kubwa kuliko yote ni hitaji la ACT la kuwepo demokrasia nchini Tanzania!
Hiki ni kichekesho! Bunge la EU hujadili masuala ya nchi wanachama. Ni sawa mtu adai Bunge la Afrika Mashariki lijadili masuala ya Izrael na Palestine na iyatolee uamuzi.
Hivi bungeni Dodoma wanajadili nini? Hivi Bunge la EU limewahi kulitaka Bunge la Tanzania lijadili maamuzi yake? Au Bunge la Tanzania likajadili masuala ya nchi mwanachama EU?
Hivi hii tabia ya kudhani Bunge la EU litaamua masuala ya Tanzania yametoka wapi? Iweje mbunge anayejinasibu kuwa msomi aonyeshe ujinga wa kiwango hiki?
Hivi hicho Chama rafiki wa ACT ni wajinga? Hawana hoja za matatizo ndani ya EU hadi wawasilishe hoja ya ACT Bunge la Ulaya? Au ndio maana hakijawahi kuwa na mbunge EU?
Au ni King Mawese anaongea uongo wake wa siku zote?

Hivi kama masuala ya Tanzania yanaongelewa na Bunge la EU Zitto huwa anaenda bungeni kujadili mambo ya nchi gani?
Upinzani huu!!!

Post Bottom Ad