Makamu wa Rais Samia awa mkali mimba za utotoni - Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

"Muda Unaongea"

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

25 Feb 2019

Makamu wa Rais Samia awa mkali mimba za utotoni

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameeleza kushitushwa na idadi ya watoto wa kike wanaopata mimba mkoani Tabora na kuagiza hatua za kuzuia tatizo hilo zichukuliwe haraka. Alisema idadi ya mimba za utotoni imeongezeka kutoka 21,889 mwaka 2017 hadi mimba 27,390 mwaka 2018.
Image result for mimba za utotoni
Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo jana wilayani Kaliua katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja vya Kolimba. Alisema kasi ya uwepo wa mimba za utotoni ni kubwa na haikubali na kutaka viongozi mkoani Tabora kubadilisha hali hiyo na kuwataka wazazi wa- jitahidikuwalinda watoto wao. Makamu wa Rais alieleza kuwa wakati mwingine wazazi hawajitokezi kutoa ushahidi pale inapojulikana watoto wao wamepata ujauzito na kwamba na kuongeza kuwa vitendo hivyo ni kuwakatili maisha yao.

Alisema kuwa hatua za makusudi zisipochukuliwa kuna uwezekano wa kuwa na wataalamu wa kike wachache kwa sababu ya kushindwa kutimiza ndoto zao. Makamu wa Rais alipongeza maandamano yaliyofanywa mkoani Tabora katika kukemea na kudhibiti mimba za utotoni akisema anatambua jitihada zinazofanywa na mkoa kudhibiti hali hiyo. Aliagiza jitihada zaidi ziongezwe kwa vile kuna ongezeko kubwa la mimba za utotoni mkoani Tabora. Makamu wa Rais anaendelea na ziara yake mkoani Tabora na ametembelea wilaya za Igunga, Nzega, Uyui na Kaliua.

Post Bottom Ad