emsuya@mwananchi.co.tz Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema alinukuliwa vibaya kuhusu mwandishi wa kujitegemea wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) mkoani Pwani, Azory Gwanda.
Profesa Kabudi ametoa ufafanuzi huo leo Alhamisi Julai 11, 2019, akidai alinukuliwa nje ya muktadha wakati akihojiwa jana katika kipindi cha Focus on Africa kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), alipoulizwa swali kuhusu kutoweka kwa Azory tangu Novemba, 2017.
Katika tamko lake kwa vyombo vya habari alilolitoa leo, Profesa Kabudi amesema, “Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki. Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti, Pwani yaliyosababisha ama watu kadhaa kupoteza maisha au kupotea.” Azory alitoweka katika mazingira ya kutatanisha kwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana ambapo mpaka sasa hajapatikana.
Waziri huyo ametoa ufafanuzi kutokana na maelezo aliyoyatoa katika kipindi cha BBC Focus on Africa ambako amekaririwa akisema Azory ni miongoni mwa wananchi waliopotea na kufariki. Alikuwa akijibu swali la mwandishi, Peter Okwoche, aliyemuuliza kuhusu kupotea kwa Azory na mahali alipo. “Hilo lilikuwa ni miongoni mwa mambo yaliyoumiza ambayo Tanzania ilipitia. Katika eneo la Rufiji, siyo Azory Gwanda peke yake aliyepotea na kufariki. Zaidi ya polisi 10 walipigwa risasi na kufariki kikatili, viongozi wengi wa vijiji wa CCM ambacho ni chama tawala, waliuawa Rufuji.”
“Tunamshukuru Mungu tuliweza kudhibiti aina hiyo ya siasa kali ambazo sasa zimehamia Kaskazini ya Msumbiji na wiki iliyopita Watanzania 10 waliuawa. Kwa hiyo Azory ni miongoni mwa Watanzania wengi waliouawa na kupotea katika eneo hilo,” amesema Profesa Kabudi katika mahojiano hayo.