Ni vyema wapiga kura na wanachama tukawajua mapema potential presidents - Yajayo Yanafurahisha | "Muda Unaongea"

top+logo

"Muda Unaongea"

Home Top Ad

jiachie

Post Top Ad

25 Mei 2018

demo-image

Ni vyema wapiga kura na wanachama tukawajua mapema potential presidents

jiachie
.com/blogger_img_proxy/
Na Yahya Msangi
Moja ya tatizo kubwa linalokabili vyama vya siasa hasa vya upinzani barani Afrika ni kutowajua wagombea wao wa uraisi mapema. Mara kadhaa husubiri hadi miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu ndio vinawatangaza utadhani mwali wa kuchezewa ngoma!
Utafiti unaonyesha kuwa hiki ndio kikwazo cha kwanza wanachojiwekea katika uchaguzi. Kuna faida nyingi zinazopatikana kwa kumjua mshika bendera mapema na hasara kibao za kutomjua hadi muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu.
Hebu tuutizame utaratibu wa marekani. Ili ugombee au uwe na nafasi ya kushinda:
Hatua ya kwanza: mgombea lazima akidhi vigezo vya kugombea uraisi - lazima athibitishe ana asili ya marekani kwa kuzaliwa. yaani lazima mgombea awe 'mmarekani' haswa. lazima awe katimiza miaka 35 kwa kuwa raisi wa marekani hawezi kuawa na umri chini ya huo. Uwe umeishi marekani kwa kipindi cha miaka 14 mfululizo. Usiwe umewahi kuhusika kuhujumu taifa au kufukuzwa na bunge. Uwe na elimu ya kutosha.Uwe walau umejihusisha na siasa.
Hatua ya pili: ili uteuliwe na chama chako kubeba bendera uongee kwanza na familia yako na wapambe wako wa karibu. Familia yako inaweza kuathirika, marafiki zako wanaweza kuathirika hivyo muhimu mkubaliane inalipa au hailipi? Uunde kamati ya kupima hali ya hewa! Utateua meneja wa kampeni. Hawa wataanza kutafuta wafadhili, wataandaa makabrasha na watataifit ni majimbo yapi muhimu kwa kampeni yako. Sio kujiendea tu kila jimbo kwa kuwa una helikopta! Utatakiwa kujisajili na tume ya uchaguzi kama mgombea ndani ya siku 15 utakapopokea au kutumia dola zaidi ya 5000. Baada ya hapo utatkiwa kutangaza rasmi wewe unagombea uraisi wa marekani. Wagombea wengi hutangaza rasmi katika jimbo walilozaliwa.
Baada ya kujitangaza unaanza rasmi kampeni na hatua ya kwanza ni kusaka hela! Walau unatakiwa uweze kupata dola bilioni 2! Sasa anza kujiuza kwa wapiga kura! Tembelea kona zote watu wakujue. Chunga kauli zako! Wengi ziliwaponza! Mfano Al Gore alijipatia sifa ya uongo baada ya kusema yeye ndio aligundua internet! Pia usitoe kauli za kuwaudhi wapiga kura na mfano ni Mitt Rooney aliyedai nusu ya wamarekani hawalipi kodi! 
Unatakiwa ushinde kura za majimbo (caucus au primary).

Hatua ya tatu: Baada ya hapo uende kwenye convention ya chama chako na ushinde! Baada ya hapo ndio kampeni kuu inaanza kati yako na wagombea wa vyama vingine. Mara nyingi mtakuwa wawili tu - democrat na republican.
Hatua ya nne: ni mbinu za kuelekea jumba jeupu yaani white house! Huu ndio wakati wa kuchunga kashfa zisikuandame! Uchunge mno ulimi wako! Ni wakati wa kuonyesha unaweza kuwa commander in chief wa US! Ndio wakati wa kutumbua kila hoja ya mwenzako! Ni wakati wa kutafuta kura za huruma! Wakati wa presidential debate onyesha wewe zaidi! Baada ya hapo subiri kuapishwa january 20 mwaka unaofuata!
Ukitizama mlolongo huu utaona kuwa kumjua mgombea wenu mapema ni jambo jema mno! Maandalizi ni mengi.
Japo Tanzania tuna utaratibu tiofauti lakini umuhimu wa kumjua mgombea wenu mapema upo pale pale. Mwaka 2015 nusura iwatumbukie nyongo CCM kutomjua mgombea wao mapema! Lakini upinzani ndio kabisaa!
Wao ndio wanatakiwa wamjue wao mapema kuliko hata CCM! Lakini nao 2015 walibaki kizani hadi dakika za lala salama wakisubiri CCM wafungue dirisha watupe wao wadake wampe bendera! Wakajikuta wamempa mtu bendera wasiyemjua sawsawa! Hakika wangemjua mapema wangembadilisha! Hakuna ambaye hakuona kuwa afya haikumudu misukosuko ya kampeni! Hakuna ambaye hakuona chama kipya hakipo moyoni kwa dhati!
Sasa 2020 CCM hawatakuwa na tatizo la kumjua mshika bendera wao! Huu ni ukweli hata kama haukufurahishi! tayari CCM wanamjua wao. Kama ana madhaifu wanajua namna ya kuyaziba. Kama ana pointi wanajua namna ya kuzikuza zijulikane kwa wapiga kura.
Je wapinzani wanamjua wao? Safari hii wapinzani wanaweza kuwa na mtihani mkubwa zaidi ya 2015.
Sisi wapiga kura tunamjua wa CCM lakini hatumjui wa CDM, CUF, NLD, TLP, NCCR au wa UKAWA!!!!!! Mtatizama wenyewe hii ina faida au hasara kwenu?
Mungu ibariki Tanzania

Post Bottom Ad

Pages